KUHUSU MRADI WETU
Kusini mwa Tanzania, hasa karibu na mpaka wa Msumbiji, ni moja ya maeneo yenye miundombinu mibovu na yenye huduma duni za kijami.
Katika hospitali chache katika eneo hili, timu ya watabibu kutoka Ujerumani hufika mara moja au mbili kwa mwaka ili kutibu watoto wenye ulemavu kama vile mguu kifundo, mdomo wazi/mdomo sungura, pamoja na upasuaji wa plastiki kwa ajili ya kurejesha ngozi katika hali yake ya kawaida baada ya majeraha yaliyotokana na kuungua, kuumia au kungatwa na wanyama.
Aina zote za nyuki hawa ni muhimu katika kuzalisha asali na kutunza nyumba zao katika mfumo wa hiraki kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Kitu kimoja cha utofauti kuhusu asali ya hawa nyuki wasiong`ata ni kwamba haifadhiwi katika mzinga wa nta kama ya nyuki wa kawaida, lakini katika vyombo vya resin vyenye umbo la puto vilivyotengenezwa kwa „tallow“ (cerumen). Hizi huipa „asali ya nyuki wasiyouma“ SBH sifa maalum.
Asali hii ni nzuri sana katika kutibu vidonda kwa sababu ya kiwango kikubwa cha antioxidants, antimicrobial na Kinga-uchochezi.
Zaidi asali hii inasaidia kuweka Ngozi katika hali ya unyevunyevu na kusaidia katika ukuzaji wa seli, hivyo kukuza ukuaji wa mishipa na oksijeni kwenye ngozi na hivyo uponyaji wa vidonda.
Kama kitu ninachofurahia kufanya, pamoja na wafugaji wa nyuki Tanzania nimeweza kufundisha wajane 9 waliopo Mikindani kwanzia mwaka 2016. Pia zaidi ya uzalishaji wa asali kutoka kwa nyuki wa wakaida, nyuki wasiong`ata wanafugwa pia na asali yao inauzwa kwenye hospitali za Ngangao na Ndanda kwa ajili ya kutibu vidonda. Shukrani kwa msaada wa kiuchumi kwa ajili ya uzalishaji wa asali na ufugaji wa nyuki yakiwemo mafunzo ya usafi na muongozo wa kupata soko yanatolewa kwa msaada wa shirika la Rotary Club Oyten››› na beekeepers association bremen››› kwa miaka kadhaa. Januari mwaka 2022, wajane 7 waliweza kufungua na kusajili Mikindani Widow Honey Cooperative.
Dr. med. Michael Fakharani, MD,
Daktari wa upasuaji wa Mifupa,
Bremen/Germany