MATIBABU YA MGUU KIFUNDO
Kote ulimwenguni, ikiwemo Tanzania, ugonjwa wa mguu kifundo hutokea kwa mtoto mmoja kati ya 800 wanaozaliwa.
Njia za matibabu zimebadilika sana katika miaka 20 iliyopita.
Mguu wa mtoto mchanga ni mlaini na unaweza kubadilishwa maumbile yake mapema, yaani katika wiki chache za kwanza za maisha kwa kutumia plasta.
Baada ya takribani matibabu matano ya ufungaji plasta, ambayo mguu wa mtoto mchanga huletwa kwa makini katika nafasi sahihi, tatizo hili la kuzaliwa na mguu usiho katika sehemu yake sahihi linaweza kurekebishwa/ kutibiwa ndani ya takribani miaka mitatu na matibabu ya uvaaji wa gangopinde (splint).
Kwa watoto au vijana ambao hawa kubahatika kutibiwa kwa wakati,upasuaji wa mguu haunabudi ufanyike baadaye.
Kwa kutumia matibabu haya operesheni hufanywa kwenye mifupa, tishu unganishi na kano.
.
Leo hii, upasuaji huu hutumiwa mara chache sana katika pande za kaskazini ya dunia.
Hata hivyo, katika nchi ya Tanzania na sehemu nyingi za Afrika, hakuna elimu juu ya
matibabu ya mapema ya ufungaji plasta ambayo si hatari.
Hii inapelekea hawa watoto, vijana, na watu wazima huteseka na ulemavu mkubwa wa kutembea katika maisha yao yote. Timu yetu ya mguu kifundo huwafanyia upasuaji watoto wakubwa hawa kwa muda wa wiki mbili bila malipo katika hospitali moja huko kusini mwa Tanzania..
Kwa vipindi vya kawaida, kila mwaka hadi miwili, wagonjwa 25 hadi 40 hutibiwa
kwa upasuaji. Madaktari wa ndani pia hufundishwa katika tiba hii.
Matibabu ya ufungaji plasta kwa watoto wachanga yamekuwa imara katika eneo lote la kusini mwa Tanzania..
Pia tumewafundisha wataalamu wa mazoezi ya viungo kuhudumia miguu kifundo kwa watoto wachanga.
Waganga wa jadi na wakunga pia wamefahamishwa kuhusu chaguo hili lamatibabu mapema.
Waganga wa jadi na wakunga pia wamefahamishwa kuhusu chaguo hili lamatibabu mapema.