MRADI WA MJANE

MRADI WA MJANE MIKINDANI TANZANIA

Katika mikoa na vijijini maskini Tanzania, wajane wengi hawana hifadhi ya kijamii.

Wanategemea tu msaada wa familia zao ambazo mara nyingi ni maskini.
Kwa kujifunza ufugaji wa nyuki, wajane hawa hupewa fursa ya kujiongezea kipato kwa kuuza asali na nta ya nyuki.
Mradi wa nyuki mjane ulianza na wajane watatu wenye umri wa miaka 30-40 ambao walikuwa na Watoto wawili na wanne mtawalia na ambao waume zao walifaraiki hasa katika ajali za barabarani.
Hawa, ambao sasa ni wajane saba, hawakuwa ma usaidizi wowote wa kifedha kutoka kwa familia zao.
Mafunzo ya ufugaji nyuki na ufadhili wa kuanzia yaliwezekana kupitia mradi wetu mwaka 2017, ili waanze ufugaji nyuki na kuuza asali yao.
Kufika mwaka 2022, tayari idadi ya wafugaji nyuki iliongezeka na kufika saba, hivyo ikaamuliwa kuanzisha akaunti ya benki ambayo wajane hao wangesimamia peke yao.
Mnamo 2022 ushirika wa asali ya wajane ya MIKINDANI ulianishwa rasmi.